Katika dunia ya kidijitali ya leo, kununua tiketi za mpira si lazima tena kusimama foleni ndefu au kuhangaika kutafuta wauzaji wa tiketi. Kupitia huduma ya N-Card, mashabiki wa michezo wanaweza sasa kulipia tiketi zao kwa njia rahisi, salama na ya haraka kwa kutumia mitandao ya simu kama Vodacom M-Pesa, Tigo Pesa (Mixx by Yas), Airtel Money, na Halopesa.
Hapa tutaelezea hatua kwa hatua jinsi ya kununua tiketi za mpira kwa kutumia kila huduma tajwa.
Faida za Kununua Tiketi kwa N-Card
- Haraka na Rahisi: Hakuna foleni, hakuna karatasi.
- Salama: Malipo ya moja kwa moja kupitia simu yako.
- Uhakika wa Tiketi: Unathibitisha tiketi papo hapo.
- Inapatikana Wakati Wowote: Huduma inapatikana saa 24

Hatua za kufata jinsi ya kununua tiketi za mpira N-Card kwa Simu
1. Jinsi ya Kununua Tiketi kwa M-Pesa (Vodacom)
Hatua za Kufuata:
- Piga
*150*00# - Chagua
4> Lipa kwa M-Pesa - Chagua
10> Zaidi - Chagua
1> e-Payment - Chagua
1> Tiketi za Michezo - Chagua
1> Tiketi za Mpira - Chagua mechi unayotaka kulipia
- Chagua kiwango cha kiingilio (aina ya tiketi)
- Weka namba ya kadi yako ya N-Card
- Ingiza namba ya siri
- Thibitisha malipo
Ujumbe wa uthibitisho utatumwa mara moja kukujulisha kuwa malipo yamefanikiwa.
2. Jinsi ya Kununua Tiketi kwa Mixx by Yas (Tigo Pesa)
Hatua za Kufuata:
- Piga
*150*01# - Chagua
4> Lipa Bill - Chagua
6> Malipo Mtandaoni - Chagua
1> Matukio Yaliyopo - Chagua
1> Tiketi za Mpira - Chagua mechi unayotaka
- Chagua aina ya tiketi
- Weka namba ya kadi ya N-Card
- Ingiza namba ya siri
- Thibitisha malipo
Ni rahisi! Uko tayari kwenda uwanjani.
3. Jinsi ya Kununua Tiketi kwa Airtel Money
Hatua za Kufuata:
- Piga
*150*60# - Chagua
5> Lipa Bill - Chagua
#kuendelea - Chagua
8> Malipo Mtandao - Chagua
1> Tiketi za Michezo - Chagua
1> Football Tickets - Chagua tukio (mechi) unayotaka
- Chagua aina ya tiketi
- Weka namba ya N-Card
- Ingiza namba ya siri
- Thibitisha malipo
Malipo yako yamekamilika na tiketi imethibitishwa.
4. Jinsi ya Kununua Tiketi kwa Halopesa
- Piga
*150*88#(nambari ya kawaida ya Halotel) - Chagua Lipa Bill > Malipo Mtandao > Tiketi za Michezo
- Fuata hatua zinazofanana:
- Chagua mechi
- Aina ya tiketi
- Ingiza Namba ya N-Card
- Thibitisha kwa PIN yako ya Halopesa
Tutahakikisha kuongeza maelezo kamili mara yanapopatikana.
Kununua tiketi za mpira kwa kutumia N-Card kupitia mitandao ya simu ni hatua kubwa ya kidijitali inayowapa mashabiki wa michezo urahisi, usalama, na uhakika wa tiketi. Bila kujali uko mkoa gani, unaweza kuwa sehemu ya mechi kubwa nchini kwa kubofya tu kwenye simu yako.
Soma pia: