Unapokosa salio lakini bado unahitaji kutumia huduma kama vile kufanya malipo au kutuma pesa kwa haraka kupitia M-Pesa, Vodacom inakuletea SongeSha—huduma inayokuwezesha kutumia M-Pesa hata kama huna salio la kutosha, halafu unalipa baadaye.
Leo tutakuonyesha hatua kwa hatua jinsi ya kujiunga na huduma ya Songesha, pamoja na mambo muhimu unayopaswa kujua.
Songesha ni nini?
SongeSha ni huduma ya mkopo wa dharura kutoka Vodacom kwa watumiaji wa M-Pesa. Inakupa uwezo wa kufanya miamala (kama kulipa bili, kutuma pesa, kununua muda wa maongezi, nk) hata kama huna salio la kutosha. Baadaye, ukishaweka pesa kwenye M-Pesa yako, deni lako linalipwa moja kwa moja.
Vigezo vya kujiunga na songesha vodacom
Kabla hujaweza kutumia Songesha, kuna vigezo vichache:
- Lazima uwe na laini ya Vodacom.
- Uwe mtumiaji wa M-Pesa kwa muda (kawaida miezi 3 au zaidi).
- Uwe na historia nzuri ya matumizi ya M-Pesa.
- Uwe na Kitambulisho sahihi (NIDA) kilichosajiliwa kwenye namba yako.
Mambo muhimu ya kufahamukabla hujajiunga songesha
- Kuna ada ndogo ya huduma ya Songesha (inategemea kiasi).
- Ukichelewa kulipa mkopo, unaweza kupunguzwa uwezo wa kukopa tena.
- Unaweza kulipa deni lako kwa kuweka salio la kutosha kwenye M-Pesa – litalipwa kiotomatiki.
Jinsi ya Kujiunga na Songesha
Hatua ni rahisi sana:
Njia ya kwanza: Kupitia *150* 00#
- Piga simu yako na dial
*150*00#
- Chagua 1. M-Pesa
- Kisha chagua 8. Huduma za ziada
- Halafu chagua 5. Songesha
- Fuata maelekezo ili kujiunga au kuangalia kama unastahili.
Njia ya pili: Kupitia App ya M-Pesa
- Fungua app ya M-Pesa kwenye simu yako.
- Ingia kwenye menyu ya “Huduma nyingine” au “More Services”.
- Chagua SongeSha.
- Bofya “Jiunge” kama hujajiunga tayari.
- Fuata maelekezo hadi mwisho.
Huduma ya Songesha ni mkombozi halisi unapokumbana na hali ya dharura. Ni rahisi, haraka, na inakuwezesha kuendelea kutumia M-Pesa bila usumbufu. Kama bado hujajiunga, fuata hatua tulizoshirikisha hapo juu na ujipatie usaidizi wa papo kwa papo kutoka Vodacom!