Kuangalia salio la NSSF ni jambo muhimu kwa wanachama ili kufuatilia michango yao na kuhakikisha akaunti zao ziko salama. Kwa mwaka 2025, NSSF imeweka njia mbalimbali za kidigitali na rahisi kwa wanachama kupata taarifa za akaunti zao kupitia simu ya mkononi, bila kulazimika kufika ofisini.
Hapa chini kuna mwongozo wa njia tatu kuu za kuangalia salio lako:
Kuangalia Salio la NSSF Kwa Njia ya SMS
- Fungua sehemu ya kutuma ujumbe kwenye simu yako.
- Andika ujumbe wenye maneno “NSSF Balance” ukifuatiwa na namba yako ya uanachama. Mfano: NSSF Balance 123456789.
- Tuma ujumbe huo kwenda namba 15200.
- Baada ya muda mfupi, utapokea ujumbe wa SMS unaoonyesha salio lako la NSSF.
Kupata Taarifa ya Statement ya Akaunti ya NSSF Kwa SMS
- Fungua sehemu ya kutuma ujumbe kwenye simu yako.
- Andika ujumbe wenye maneno “NSSF Statement” ukifuatiwa na namba yako ya uanachama. Mfano: NSSF Statement 123456789.
- Tuma ujumbe huo kwenda namba 15200.
- Utapokea taarifa ya statement ya akaunti yako ikionyesha michango yote na salio lililopo.
Kuangalia Salio la NSSF Kupitia WhatsApp
- Hifadhi namba 0756 140 140 kwenye simu yako.
- Fungua WhatsApp na tuma ujumbe “Hello” au “Habari”.
- Fuata maelekezo yanayojitokeza ili kuangalia salio lako (Balance) au taarifa za michango (Statement).
Kuangalia Salio la NSSF kwa Programu ya Simu “Janja”
- Pakua programu ya “NSSF Taarifa” kutoka Google Play Store.
- Ingia kwa kutumia maelezo yako ya NSSF (namba ya uanachama).
- Angalia salio lako, michango yote, na taarifa nyingine muhimu kuhusu akaunti yako.
Soma pia: