Wamiliki wa ardhi nchini Tanzania sasa wanaweza kuangalia deni la kodi ya ardhi (Land Rent) kwa urahisi kupitia huduma za mtandaoni zinazotolewa na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi. Mfumo huu umeundwa ili kurahisisha huduma na kuondoa usumbufu wa kwenda ofisini.
Kwa Kutumia Huduma za Mtandaoni
1. Tembelea tovuti ya Wizara ya Ardhi
- Fungua tovuti rasmi ya huduma za kodi ya ardhi: https://landrent.lands.go.tz
- Kwenye ukurasa mkuu, tafuta kipengele cha “Kadiria Kodi ya Ardhi.”
- Bonyeza sehemu hiyo ili kuendelea na mchakato.
2. Ingiza Taarifa za Kiwanja Chako
- Mfumo utakutaka uingize taarifa kama:
- Namba ya Hati ya Ardhi (Title Number)
- ID ya Kiwanja (Plot ID) au
- Taarifa nyingine za Kiwanja
- Hii itasaidia mfumo kupata taarifa sahihi kuhusu mmiliki na deni lililopo.
3. Chagua Mkoa na Wilaya
- Baada ya kuingiza taarifa, chagua mkoa na wilaya ambapo kiwanja chako kilipo.
- Hatua hii inahakikisha kuwa mfumo unatafuta taarifa zako kwenye eneo sahihi la mamlaka ya ardhi.
4. Pokea Makadirio ya Deni
- Baada ya kuthibitisha taarifa zako, mfumo utaonesha kiasi cha deni la kodi ya ardhi unachodaiwa pamoja na maelekezo ya jinsi ya kulipa.
- Unaweza kuchapisha (print) makadirio hayo au kuhifadhi kama ushahidi wa malipo yako.
Soma pia: