MDAs (Wizara, Idara na Taasisi za Serikali) pamoja na LGAs (Mamlaka za Serikali za Mitaa) wametangaza nafasi 492 za kazi za Daktari Daraja la II (Medical Officer II) kupitia Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma. Nafasi hizi zinalenga kuimarisha huduma za afya katika hospitali na vituo vya afya vya umma nchini.
Waombaji wote wenye sifa wanakaribishwa kutuma maombi yao kwa kuzingatia masharti na vigezo vilivyowekwa kwenye tangazo rasmi la ajira kupitia mfumo wa Ajira Portal. Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 27/02/2026. Waombaji wanashauriwa kuwasilisha maombi mapema kabla ya muda wa mwisho ili kuepuka usumbufu wa mfumo.
Majukumu ya Kazi
- Kufanya kazi zote za matibabu hospitalini zinazohusiana na magonjwa mbalimbali yakiwemo magonjwa ya watoto, magonjwa ya akina mama na upasuaji wa kawaida na wa dharura.
- Kutoa na kusimamia elimu ya afya pamoja na kuboresha afya ya jamii katika Wilaya na Mikoa au eneo lake la kazi.
- Kuchunguza, kufuatilia na kuzuia milipuko ya magonjwa.
- Kutunza takwimu na kuzitumia kama inavyoelekezwa katika misingi ya MTUHA.
- Kupanga na kutathimini huduma za afya katika eneo lake la kazi.
- Kufundisha wanafunzi na watumishi waliopo kwenye eneo la kazi.
- Kusimamia na kuelekeza wafanyakazi walio chini yake.
- Kubuni na kuendesha utafiti na kusambaza matokeo.
- Kubuni na kutayarisha mikakati ya kuinua ubora wa huduma ya fani yake.
- Kuandaa mipango na makisio ya bajeti ya huduma za afya.
- Kushiriki, kuhakiki na kuboresha huduma za afya (medical audit and quality improvement).
Vigezo na Elimu
Kuajiriwa wenye Shahada ya Udaktari kutoka Vyuo Vikuu/Vyuo vinavyotambuliwa na Serikali waliomaliza “Internship” na kupata usajili kutoka Baraza la Madaktari Tanganyika (Medical Council of Tanganyika).