Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Secretariat ya Ajira kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, imetangaza rasmi Nafasi mpya za kazi za ualimu kwa mwaka 2025. Ajira hizi zinahusisha walimu wa madaraja yote ikiwemo Daraja III A, Daraja III B, na Daraja III C, ikiwa ni sehemu ya juhudi za serikali kuboresha sekta ya elimu na kupunguza upungufu wa walimu katika shule za msingi na sekondari nchini.
Walimu wa Madaraja Yote Wamenufaika
Katika tangazo hilo, serikali imesisitiza kuwa nafasi hizo ni kwa walimu wa ngazi tofauti, ikiwemo:
- Walimu wa Daraja III A: Wanaofundisha shule za msingi.
- Walimu wa Daraja III B: Wanaofundisha shule za sekondari, hasa masomo ya sayansi, hisabati, na lugha.
- Walimu wa Daraja III C: Walimu wa ufundi na elimu maalum.
Kwa kuzingatia vigezo vilivyowekwa, walimu wote waliomaliza mafunzo yao katika vyuo vinavyotambulika na Serikali wanahimizwa kuwasilisha maombi yao kupitia mfumo wa Ajira Portal (www.ajira.go.tz).