Huduma ya kukopa salio YAS (Tigo) huwasaidia wateja wa Tigo kuendelea kupiga simu, kutuma SMS au kutumia intaneti pale salio linapoisha ghafla. Huduma hii ni rahisi kutumia na inapatikana moja kwa moja kupitia simu ya mkononi bila kuhitaji intaneti. Kwa kufahamu jinsi ya kukopa salio YAS (Tigo), utaepuka usumbufu wa kukosa mawasiliano muhimu.
Hatua za Kukopa Salio Tigo
Ili kufanikisha kukopa salio YAS (Tigo), fuata hatua hizi kulingana na huduma unayohitaji:
- Piga *149*05# na chagua kifurushi unachotaka kuazima, iwe ni dakika, SMS au MB za intaneti.
- Piga *149*49# endapo unahitaji kukopa dakika za kupiga simu.
- Piga *149*55# ili kukopa MB za kuperuzi intaneti.
- Piga *147*00# kwa kifurushi kinachojumuisha dakika, SMS na MB kwa pamoja.
Baada ya kuchagua kifurushi, thibitisha ombi lako kwa kufuata maelekezo yatakayoonekana kwenye simu yako.
Huduma ya kukopa salio YAS (Tigo) hutegemea matumizi ya laini yako na historia ya ulipaji wa mikopo ya awali. Kadri unavyolipa kwa wakati, ndivyo unavyoongeza uwezekano wa kukopa tena kiasi kikubwa zaidi.
Soma pia: Jinsi ya kukopa Bustisha Tigo YAS