Ratiba ya mechi za Simba SC katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika kwa msimu wa 2025/2026 inatoa changamoto kubwa kwa timu hiyo, kwani inajumuisha mechi dhidi ya baadhi ya vilabu bora barani Afrika. Simba, ikiwa ni moja ya klabu zinazoshikilia hadhi kubwa kwenye soka la Afrika Mashariki, itashiriki kwa mara nyingine katika hatua za makundi. Ratiba hiyo itahusisha mechi za nyumbani na ugenini, ambapo Simba itakuwa na jukumu la kuhakikisha inapata matokeo chanya, hasa nyumbani, ili kujihakikishia nafasi ya kuendelea mbele katika mashindano.
Mashabiki wa timu hiyo wanatarajiwa kuwa bega kwa bega na wachezaji, kwa kushika moto viwanja vya Dar es Salaam na ugenini. Lengo kuu la Simba ni kutwaa taji la Klabu Bingwa Afrika, jambo ambalo linahitaji maandalizi makini, umoja, na ari ya hali ya juu kutoka kwa wachezaji, benchi la ufundi, na mashabiki wake.

Ratiba ya mechi za Simba Makundi kimataifa Klabu Bingwa 2025/2026
November 21, 2025: Simba sc vs Petro de Luanda
November 28, 2025: Stade de Malien vs Simba sc
January 23, 2026: ES Tunis vs Simba sc
January 30, 2026: Simba sc vs ES Tunis
February 6, 2026: Petro de Luanda vs Simba sc
February 13, 2026: Simba sc vs Stade de Malien
Soma pia: