Mechi ya hatua ya awai ya ligi ya mabingwa (CAF CL) kati ya Yanga sc vs Wiliete sc itakayochezwa 06:00 pm huko Angola.
Leo ni siku muhimu kwa Yanga SC wanapomenyana na Wiliete sc katika mchezo wa kwanza wa awali wa kuwania kufuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF Champions League). Huu ni mchezo wa kwanza kati ya miwili ambao utaamua hatma ya timu hizi katika safari yao ya kuingia hatua ya makundi ya michuano hiyo mikubwa barani Afrika.
Yanga SC, mabingwa wa Tanzania, wamejiandaa kwa umakini mkubwa kupitia mazoezi ya kina, kambi maalum na mikakati ya kiufundi inayolenga kupata matokeo mazuri ugenini. Benchi la ufundi limeweka mkazo kwenye nidhamu ya uwanjani, uimara wa safu zote, pamoja na uzoefu wa kimataifa kuhakikisha wanajilinda vyema na kushambulia kwa ufanisi.
Kwa upande wa Wiliete sc, wakiwa nyumbani, wamejiandaa kwa ari na morali ya juu. Timu hiyo kutoka Angola imekuwa ikijifua vikali, ikilenga kutumia faida ya uwanja wa nyumbani – The Estadio 11 de Novembro – ambao ni mmoja wa viwanja bora kabisa Afrika, ili kupata matokeo yatakayowapa nafasi nzuri kuelekea mchezo wa marudiano.
Mashabiki wa soka barani Afrika wanatarajia mchezo wa ushindani mkubwa, wenye kasi, mbinu na nidhamu ya hali ya juu kutoka kwa timu hizi mbili zenye historia tofauti lakini malengo yanayofanana – kufika hatua ya makundi ya CAFCL.
Soma pia: