Ratiba ya Ligi Kuu NBC Tanzania Bara kwa msimu wa 2025–2026 imeanza rasmi tarehe 17 Septemba 2025, ikihusisha timu 16 kushindana kwa mfumo wa mikwaju ya nyumbani na ugenini (home and away)
Mechi ya ufunguzi itakuwa kati ya KMC FC na Dodoma Jiji, itakayopigwa katika Uwanja wa KMC Complex jijini Dar es Salaam. Msimu huu unatarajiwa kuwa wa kusisimua, huku timu zote 16 zikipambana kwa mfumo wa ligi ya nyumbani na ugenini. Moja ya mechi zinazovutia zaidi katika ratiba hiyo ni Kariakoo Derby, inayozikutanisha mahasimu wa jadi, Simba SC na Yanga SC. Mechi ya kwanza ya watani hao wa jadi itachezwa tarehe 13 Desemba 2025, huku mzunguko wa pili wa pambano hilo ukipangwa kufanyika tarehe 4 Aprili 2026. Mashabiki wa soka nchini wanatarajia msimu wenye ushindani mkubwa, haswa kutoka kwa timu kubwa pamoja na zile zinazopambana kuepuka kushuka daraja.
Ratiba ya NBC Premier League Tanzania Bara Msimu wa 2025 2026










Soma pia: