Kuwa na intaneti ya uhakika nyumbani ni jambo muhimu hasa katika dunia ya sasa. Airtel Tanzania inatoa huduma ya Router WiFi inayokuwezesha kupata intaneti ya kasi bila usumbufu. Ikiwa tayari una router ya Airtel, swali kuu huwa unawezaje kulipia kifurushi cha intaneti?
Jinsi ya kulipia airtel Router 5g
Hapa chini tumeandaa mwongozo rahisi utakao kusaidia kulipia huduma hiyo haraka, bila kutumia muda mwingi.
Jinsi ya kulipia Airtel Router 5G wifi Kupitia Airtel Money
Hii ndiyo njia rahisi na ya moja kwa moja:
Hatua za kufuata:
- Fungua menyu ya Airtel Money kwa kubonyeza
*150*60#
- Chagua Intaneti & Vifurushi
- Chagua WiFi Router
- Ingiza namba ya router (IMEI au namba maalum ya WiFi)
- Chagua kifurushi unachotaka
- Thibitisha malipo kwa PIN yako.
Kulipia Airtel Router WiFi ni rahisi kuliko unavyofikiria. Ukiwa na Airtel Money, App ya My Airtel au hata huduma za benki, unaweza kujaza kifurushi chako cha WiFi kwa sekunde chache tu. Hakikisha una namba sahihi ya Router kabla ya kufanya malipo ili kuepuka usumbufu.
Soma pia: