Kama unatumia Azam TV kufuatilia burudani za nyumbani, michezo au vipindi vya watoto, ni muhimu kujua namna rahisi ya kulipia kifurushi chako bila usumbufu. Hapa chini tumekuandalia mwongozo kamili wa jinsi ya kulipia Azam TV kwa kutumia mitandao ya simu ya Vodacom, Airtel, Halotel na Yas.
Jinsi ya Kulipia Azam TV kwa mitandao yote ya simu
Kuna njia mbalimbali rahisi na salama zinazokuwezesha kulipia kifurushi cha Azam TV moja kwa moja kupitia simu yako ya mkononi. Huduma hii imeboreshwa ili kukidhi mahitaji ya watumiaji wa mitandao yote mikubwa ya simu hapa Tanzania – ikiwemo Vodacom, Airtel, Halotel na Yas
Jinsi ya Kulipia King’amuzi cha Azam tv kwa M-Pesa:
- Piga *150*00#
- Chagua Lipa kwa M-Pesa
- Chagua Namba 4 – Malipo ya Kampuni
- Chagua Namba 3 – Chagua Kwenye Orodha
- Chagua Namba 1 – King’amuzi
- Chagua Namba 5 – Azam TV
- Weka namba ya kadi
- Chagua bei ya kifurushi unachotaka
- Weka Namba ya Siri
- Bonyeza 1 kuthibitisha
Jinsi ya Kulipia King’amuzi cha Azam TV kwa Airtel Money:
- Piga *150*60#
- Chagua Lipa Bili
- Chagua “Chagua Kampuni”
- Chagua “TV Ving’amuzi”
- Chagua “Azam”
- Weka namba ya kadi ya Azam
- Weka kiasi
- Bonyeza 1 Kukubali
- Weka Pini yako
Jinsi ya Kulipia King’amuzi cha Azam TV kwa Tigo Pesa / Mixx by Yas:
- Piga *150*01#
- Chagua “Lipa Bili”
- Chagua “Kupata majina ya kamapuni”
- Chagua “King’amuzi”
- Chagua “Azam Pay TV”
- Weka Kumbukumbu Namba (Akaunti ya Azam TV)
- Ingiza kiasi
- Ingiza namba ya siri kuhakiki
Jinsi ya Kulipia King’amuzi cha Azam TV kwa Halopesa:
- Piga *150*88#
- Chagua “Lipa Bili”
- Chagua “Kifurushi cha Azam TV”
- Weka kiasi cha malipo unachotaka kulipa
- Ingiza Namba ya Marejeleo ya Akaunti yako ya Azam TV
- Weka Pini yako ya Halotel
- Bonyeza 1 ili kuthibitisha malipo
Faida za Kulipia Azam TV kwa Simu:
- Haraka na rahisi
- Hakuna foleni
- Malipo salama kwa njia ya simu
- Unapokea uthibitisho papo hapo
Sasa unajua jinsi ya kulipia kifurushi cha Azam TV online kwa kutumia Vodacom, Airtel, Halotel au Yas. Hakikisha unafanya malipo kabla kifurushi kuisha ili kuepuka kukosa vipindi unavyovipenda.
Soma pia: