Hatua kwa hatua Jinsi ya Kulipia Simu ya Mkopo Watu Credit kwa mitandao yote ya Simu kama M-pesa, Airtel Money, Mixx By Yas na Halopesa
Watu Credit ni moja kati ya taasisi zinazotoa mikopo ya simu kwa urahisi na uharaka nchini Tanzania. Ili kuhakikisha unaendelea kutumia kifaa chako bila usumbufu, ni muhimu kulipa mkopo kwa wakati. Blogi hii itakuonyesha jinsi ya kulipia mkopo wa simu kutoka Watu Credit kwa kutumia huduma kuu za malipo za simu: M-Pesa, Mixx by Yas, Airtel Money na Halopesa.
Hatua za Kulipia Mkopo wa Simu Watu Credit – M-Pesa, Mixx by Yas, Airtel Money, Halopesa
Fuatisha hatua zifuatazo kulipia mkopo wako wa simu:
Jinsi ya Kulipia Kupitia M-Pesa (Vodacom)
- Piga *150*00#
- Chagua 4. Lipa kwa M-Pesa
- Chagua 5. Lipa Bili
- Chagua 1. Ingiza namba ya kampuni
- Ingiza 650880
- Ingiza Namba yako ya simu kama Kumbukumbu
- Ingiza kiasi unachotaka kulipa
- Weka PIN yako ya M-Pesa na thibitisha muamala
Jinsi ya Kulipia Kupitia Mixx by Yas (Tigo)
- Piga *150*01#
- Chagua 4. Lipa Bili
- Chagua Ingiza Namba ya Kampuni
- Andika 650880
- Weka namba yako ya simu kama kumbukumbu
- Andika kiasi
- Weka PIN yako ya Mixx by Yas
- Thibitisha malipo yako
Jinsi ya Kulipia Kupitia Airtel Money
- Piga *150*60#
- Chagua 5. Lipa Bili
- Chagua 1. Weka Namba ya Kampuni
- Andika 650880
- Weka namba yako ya simu (iliyopata mkopo) kama kumbukumbu
- Ingiza kiasi cha kulipa
- Weka PIN yako ya Airtel Money
- Thibitisha
Jinsi ya Kulipia Kupitia HaloPesa (Halotel)
- Piga *150*88#
- Chagua 5. Lipa Bili
- Chagua 1. Weka namba ya kampuni
- Andika 650880
- Ingiza namba yako ya simu kama kumbukumbu
- Weka kiasi cha kulipa
- Ingiza PIN yako ya HaloPesa
- Thibitisha muamala
Vidokezo Muhimu vya Kulipa Mkopo Watu Credit
- Hakikisha namba ya kampuni ni sahihi: 650880
- Tumia namba ya simu uliyojisajilia nayo mkopo kama kumbukumbu
- Lipia mkopo wako kwa wakati ili kuepuka tozo za ziada au kudhoofisha historia yako ya kifedha
- Unaweza kulipa kiasi chote au sehemu kulingana na makubaliano yako na Watu Credit
Kwa Msaada Zaidi:
Ikiwa unakutana na changamoto yoyote wakati wa kufanya malipo, unaweza kuwasiliana moja kwa moja na huduma kwa wateja wa Watu Credit kupitia namba ya simu au barua pepe iliyopo kwenye tovuti yao rasmi.
Kulipa mkopo wa simu kutoka Watu Credit ni rahisi, salama na haraka kupitia huduma za malipo za simu kama M-Pesa, Mixx by Yas, Airtel Money na HaloPesa. Fuata hatua zilizoelekezwa katika mwongozo huu kuhakikisha unakamilisha muamala wako kwa mafanikio.
Soma pia:
- Jinsi ya Kulipia Ada na Faini za TARURA (Magesho na Parking za Magari)
- Bei ya Vifurushi vya DSTV 2025 – Siku, Wiki & Mwezi
- Bei ya Vifurushi vya Azam TV Tanzania 2025 – Siku, Wiki & Mwezi