Jeshi la Magereza Tanzania Bara, kupitia Kamishna Jenerali Jeremiah Katungu, limetangaza rasmi mnamo Agosti 15, 2025, Tangazo la ajira kwa vijana wa Kitanzania waliohitimu kidato cha nne au wenye shahada na stashahada katika fani mbalimbali kama Uhandisi wa Programu, Usalama wa Mifumo, Sayansi ya Teknolojia Mseto, Uhandisi wa Mitandao, Saikolojia na Ushauri, Uhandisi wa Uchimbaji Madini, pamoja na stashahada katika Uuguzi, Kilimo, Mifugo, Ufundi wa Vifaa vya Ofisi, Lugha za Alama, na Katibu Muhtasi.
BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD TANGAZO LA KAZI MAGEREZA
Maombi ya nafasi hizi yanapaswa kuwasilishwa kupitia mfumo rasmi wa Tanzania Prisons Service Recruitment Management System (TPSRMS), kabla ya tarehe ya mwisho ya kuwasilisha maombi ambayo ni Agosti 29, 2025. Tangazo hili linaweka mkazo kwenye uwazi, usawa, na matumizi ya teknolojia katika kuendesha mchakato wa ajira serikalini.
Soma pia: Nafasi za Kazi Jeshi la Magereza 2025