Unatafuta fomu za kujiunga na vyuo vya afya Tanzania kwa mwaka wa masomo 2025/2026? Iwe umepangiwa na NACTVET au umechaguliwa moja kwa moja na chuo, makala hii itakuongoza namna ya kupata joining instructions, kujua mahitaji ya msingi, na viungo rasmi vya vyuo vya afya nchini.
Vyuo vya Afya Tanzania
Vyuo vya afya hutoa mafunzo kwa kada mbalimbali kama:
- Uuguzi (Nursing)
- Maabara (Laboratory Sciences)
- Dawa (Pharmaceutical Sciences)
- Tabibu (Clinical Medicine)
- Radiolojia (Radiology)
- Meno, Afya ya Jamii, n.k.
Vyuo hivyo hujumuisha vyuo vya serikali na binafsi, vinavyosimamiwa na NACTVET chini ya Wizara ya Afya.
FOMU ZA KUJIUNGA NA VYUO VYA AFYA ZINAPATIKANA KATIKA TOVUTI RASMI ZA CHUO
Kupata fomu za kujiunga na vyuo vya afya ni hatua muhimu kwa kila mwanafunzi aliyechaguliwa kujiunga. Hakikisha unapakua fomu hiyo kutoka kwenye tovuti rasmi, unasoma kwa makini na kuandaa kila unachohitajika nacho kabla ya tarehe ya kuripoti.
Soma pia: