Katika dunia ya leo, ni muhimu sana kuhakikisha unafanya biashara au kushirikiana na kampuni halali, iliyosajiliwa kisheria. Tanzania kupitia BRELA (Business Registrations and Licensing Agency), imeanzisha mfumo wa mtandao unaokuwezesha kuangalia usajili wa kampuni BRELA kwa urahisi, bila kwenda ofisini. Kupitia makala hii, tutakuonyesha hatua kwa hatua jinsi ya kukagua usajili wa kampuni kupitia Online Registration System (ORS).
BRELA ni wakala wa usajili wa biashara na leseni nchini Tanzania. Miongoni mwa majukumu yake ni:
- Kusajili kampuni
- Kusajili majina ya biashara
- Kutoa leseni za biashara
- Kuweka kumbukumbu za umiliki na mabadiliko ya kampuni
Kupitia mfumo wa ORS (Online Registration System), huduma zote hizi sasa zinaweza kufanyika mtandaoni.
Kwa Nini Uangalia Usajili wa Kampuni BRELA?
- Kuhakikisha kampuni unayoshirikiana nayo imesajiliwa kihalali
- Kuthibitisha jina, aina ya kampuni, wamiliki na anwani rasmi
- Kuepuka udanganyifu wa kibiashara
- Mahitaji ya kisheria au usalama wa biashara yako
Jinsi ya Kuangalia Usajili wa Kampuni BRELA (ORS)
Ili kukagua usajili wa kampuni yoyote, fuata hatua hizi:
Hatua ya 1: Tembelea Tovuti ya BRELA Nenda kwenye https://ors.brela.go.tz/
Hatua ya 2: Bonyeza “Public Search” Tovuti ya ORS ina sehemu inayoitwa Public Search, ambayo hukuwezesha kutafuta taarifa za kampuni hata bila akaunti.
Hatua ya 3: Ingiza Jina la Kampuni au TIN
Katika kisanduku cha kutafuta, weka:
- Jina la kampuni (kama vile ABC Limited)
- Au Namba ya TIN ikiwa unayo
Hatua ya 4: Angalia Matokeo
Mfumo utakuletea taarifa hizi:
- Jina kamili la kampuni
- Namba ya usajili
- Tarehe ya usajili
- Aina ya kampuni (Private/Public)
- Anwani ya ofisi
- Wamiliki/wakurugenzi
- Hali ya usajili (Active/Inactive)
Kuangalia usajili wa kampuni BRELA ni hatua muhimu kwa wafanyabiashara, wawekezaji, wanunuzi na hata wateja wanaotaka kuhakikisha wanahusika na taasisi halali. Kwa kutumia mfumo wa ORS, unaweza kupata taarifa sahihi kwa sekunde chache tu bila malipo.
Mapendekezo ya Mhariri: