Kuandika barua ya uhamisho ni hatua muhimu sana kwa mwalimu anayehitaji kuhamia shule au kituo kingine. Ili barua yako ikubalike haraka, ni muhimu kuandika kwa lugha rasmi na kufuata muundo sahihi. Katika blogu hii, utajifunza:
- Sababu kuu za uhamisho wa walimu
- Muundo sahihi wa barua ya uhamisho
- Mfano wa barua ya uhamisho wa mwalimu unaoweza kutumia kama kigezo
Mfano wa Barua ya Uhamisho wa Mwalimu
[Tarehe]
Kwa: Afisa Elimu Wilaya,
[Anwani ya Ofisi]
YAH: OMBI LA UHAMISHO
Ndugu Afisa Elimu,
Mimi ni [Jina Kamili], mwalimu wa [somu unalofundisha] katika shule ya [Jina la Shule] tangu mwaka [Mwaka]. Napenda kuwasilisha ombi langu la kuhamishwa kutoka kituo hiki hadi [Jina la Shule au Wilaya Unayotaka], kutokana na [Sababu fupi].
Naomba ombi hili lishughulikiwe kwa wakati ili niweze kuendelea na majukumu yangu kwa ufanisi.
Wako kwa uaminifu,
[Jina Kamili]
[Mwalimu wa – somo au darasa]
[Namba ya Simu]
[Sahihi]
Kuandika barua ya uhamisho kwa njia sahihi kunaongeza nafasi ya ombi lako kukubaliwa. Tumia huu mfano wa barua ya uhamisho wa mwalimu kama kielelezo ili kuhakikisha umefuata taratibu zote za kitaaluma.
Mapendekezo ya mhariri: