Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) limetangaza Matokeo ya Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi (PSLE) kwa mwaka 2026, yaliyofanyika mwezi Septemba 2026. Matokeo hayo yametangazwa leo, tarehe 03 Novemba 2026, na yanapatikana kupitia tovuti rasmi ya Baraza la Mitihani la Tanzania.
Wanafunzi waliofanya mtihani wa Darasa la Saba mwaka 2026, pamoja na wazazi na walezi wao, sasa wanaweza kuangalia matokeo yao ili kufahamu kiwango cha ufaulu wa watahiniwa na kujua hatua inayofuata katika safari yao ya elimu.

Kupitia makala hii, tumekuandalia mwongozo wa jinsi ya kuangalia Matokeo ya Darasa la Saba 2026 (NECTA PSLE Results 2026) kwa kutumia simu au kompyuta kupitia mtandao.
Jinsi ya Kuangalia Matokeo ya Darasa la Saba 2026
Ili kuangalia matokeo yako ya Darasa la Saba 2026, fuata hatua zifuatazo:
- Tembelea tovuti rasmi ya NECTA kupitia https://www.necta.go.tz.
- Bofya sehemu ya Results.
- Chagua PSLE (Primary School Leaving Examination).
- Chagua mwaka wa mtihani 2026.
- Chagua mkoa ambao mwanafunzi alifanyia mtihani.
- Chagua wilaya au halmashauri husika.
- Chagua jina la shule aliyosoma mwanafunzi.
- Tafuta jina au namba ya mtihani ya mwanafunzi ili kuona matokeo yake.
Link ya Kuangalia Matokeo ya Darasa la Saba 2026
Wanafunzi na wazazi wanaweza kutumia kiungo rasmi cha NECTA hapa chini kufungua ukurasa wa matokeo ya mtihani wa Darasa la Saba.
ANGALIA MATOKEO YA DARASA LA SABA 2026 HAPA:
https://www.necta.go.tz/results/view/psle
Endelea kutembelea tovuti yetu kwa taarifa zaidi kuhusu Matokeo ya Darasa la Saba 2026, pamoja na majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Kwanza 2027.