CAF imeendesha droo ya hatua ya awali ya mashindano ya klabu bingwa Afrika (CAFCL) na kombe la shirikisho (CAFCC) msimu wa 2025/26. Tanzania inawakilishwa na vilabu vinne: Simba SC na Yanga SC kwenye CAF Champions League, huku Azam FC na Singida Big Stars wakicheza kwenye CAF Confederation Cup.
Hatua ya Awali ya CAF Champions League 2025/26: Simba SC & Yanga SC
Mfumo wa Droo Ulivyofanyika
Droo rasmi ya hatua ya awali ya CAF Champions League 2025/26 ilifanyika tarehe 9 Agosti 2025, jijini Dar es Salaam, Tanzania. Klabu zote zilizotimiza masharti ya CAF ziliorodheshwa kwenye vikundi vinavyoitwa “Pots”, kulingana na alama za viwango vya CAF (CAF Club Ranking) pamoja na kijiografia.
- Timu zenye alama za juu zilipangiwa kupokea wapinzani kutoka Pot ya chini.
- Mechi hizi zitachezwa kwa mikondo miwili (nyumbani na ugenini).
Simba SC na Yanga kwenye Klabu Bingwa (CAF Champions League)
Simba sc vs Gaborone utd
Yanga sc vs Wiliete Benguela
Ratiba Muhimu CAFCL
- Hatua ya Awali (First Round):
Leg 1: Septemba 19–21, 2025
Leg 2: Septemba 26–28, 2025 - Hatua ya Pili (Second Round):
Leg 1: Oktoba 17–19, 2025
Leg 2: Oktoba 24–26, 2025
Hatua ya Awali ya CAF Confederation Cup 2025/26: Azam FC & Singida Big Stars
Katika droo ya CAF Confederation Cup 2025/26, jumla ya vilabu 58 vilishiriki. Timu kadhaa zilipata bye moja kwa moja hadi hatua ya pili, lakini Azam FC na Singida Big Stars zinatakiwa kushiriki hatua ya awali.
Zimewekwa kwenye Pot 2, na zitapangwa dhidi ya timu kutoka Pot nyingine (Pot 1 au 3) kwa kuzingatia alama na kijiografia.
Azam na Singida Big Stars kwenye Kombe la shirikishio (CAFCCL)
Azam Fc vs El Merrikh Bentiu
Singida Big stars vs Rayon Sports
Ratiba Muhimu CAFCC
- Hatua ya Awali (First Round):
Leg 1: Septemba 19–21, 2025
Leg 2: Septemba 26–28, 2025 - Hatua ya Pili (Second Round):
Leg 1: Oktoba 17–19, 2025
Leg 2: Oktoba 24–26, 2025
Kwa msimu huu wa 2025/26, Tanzania inawakilishwa vyema na klabu nne zenye uwezo mkubwa wa kusababisha maajabu Afrika. Hatua ya awali ndiyo mwanzo wa safari ngumu lakini yenye matumaini. Mashabiki, wadau wa soka, na taifa kwa ujumla, waendelee kutoa sapoti.
Soma pia: Viwango vya Ubora CAF 2025: Simba yapanda hadi nafasi 5