Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia (MoEST) imetangaza rasmi nafasi za kujiunga na Mafunzo ya Ualimu ya Stashahada kwa ngazi za Elimu ya Awali na Msingi (Miaka 02) pamoja na Stashahada ya Ualimu Maalumu ya Ualimu Elimu ya Msingi (Miaka 03) katika masomo ya Sayansi na Hisabati.
SIFA ZA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA UALIMU
- Sifa za kujiunga na Stashahada ya Ualimu Elimu ya Awali na Msingi (Miaka 02) ni:
- Wahitimu wa Kidato cha sita wenye ufaulu wa Daraja la I-III kwa kiwango cha “Principal Pass” mbili (02). Aidha, kwa waombaji waliosomea masomo ya Economics, Commerce na Book Keeping waombe kozi ya Stashahada ya Ualimu
wa Elimu ya Awali. - Walimu waliohitimu Mafunzo ya Ualimu Ngazi ya Astashahada (Cheti) ya Ualimu Elimu ya Awali au Msingi. Aidha waombaji wa mafunzo watakaochaguliwa, watapangwa kwenye mikondo kulingana na ufaulu wao katika Mtihani wa Taifa wa Ualimu ngazi ya Astashahada ya Elimu ya Ualimu.
- Wahitimu wa Kidato cha sita wenye ufaulu wa Daraja la I-III kwa kiwango cha “Principal Pass” mbili (02). Aidha, kwa waombaji waliosomea masomo ya Economics, Commerce na Book Keeping waombe kozi ya Stashahada ya Ualimu
- Sifa za kujiunga na Stashahada Maalumu ya Ualimu Elimu ya Msingi (Miaka 03) ni wahitimu wa Kidato cha nne wenye ufaulu wa Daraja la I-III kwa kiwango cha alama “C” au zaidi katika masomo matatu, mawili kati yake yakiwa ni: Basic
Mathematics, Biology, Chemistry, Physics, Information and Computer Studies au Computer Science..