Kulipa simu ya mkopo Watu Credit ni rahisi na unaweza kufanya malipo kupitia huduma mbalimbali za kielektroniki kama M-Pesa, Airtel Money, Mixx by Yas (Tigo Pesa), au Halopesa.
Jinsi ya Kulipia Simu ya Mkopo watu credit kwa kutumia mitandao ya Simu M-pesa, Airtel money, Mixx by Yas (Tigo pesa) na Halopeda
Hapa chini ni hatua rahisi za kufuata:
- Fungua Menu ya huduma yako ya fedha za simu:
- Fungua M-Pesa, Airtel Money, Mixx by Yas, au Halopesa kwenye simu yako.
- Chagua Sehemu ya Kulipia kwa Namba ya Kampuni:
- Katika menu, tafuta chaguo linalosema “Lipa kwa Namba ya Kampuni” au “Pay Bill”.
- Weka Namba ya Kampuni ya Watu Credit:
- Weka namba ya kampuni: 650880.
- Weka namba ya Kumbukumbu
- Utaweka Namba yako ya Simu uliyojiungia kwenye watu credit
- Weka Kiasi cha Malipo:
- Weka kiasi unachotaka kulipa kulingana na deni lako la simu ya mkopo.
- Thibitisha kwa Kuweka Neno la Siri:
- Weka neno la siri la huduma yako ya simu pesa ili kuthibitisha malipo.
Baada ya kuthibitisha, utapokea ujumbe wa uthibitisho wa malipo. Hakikisha unahifadhi ujumbe huu kama kumbukumbu ya malipo yako.
Soma pia: