Michuano ya CHAN 2025 imeendelea kwa kasi, na hatua ya makundi imetoa wachezaji wengi wa kustaajabisha kutoka nchi mbalimbali barani Afrika. Baada ya mechi chungu nzima za awali, wachezaji hawa wameonyesha kiwango bora na kuunda kikosi bora cha hatua ya makundi. Hapa chini ni orodha ya wachezaji waliopata alama za juu kwa nafasi zao:
Kikosi Bora cha Hatua ya Makundi (Group Stage)
- Ladji Brahima Sanou (Burkina Faso): 7.9
- Mohamed Réda Halaïmia (Algeria): 7.5
- Mohamed Husseini (Tanzania): 9.5
- Ayoub Ghezala (Algeria): 8.5
- Alphonce Omija (Kenya): 8.3
- Walieldin Khidir (Sudan): 7.8
- Moussa Cissé (Senegal): 8.0
- Mohamed Bangoura (Guinea): 7.9
- Abderrahmane Meziane (Algeria): 9.0
- Austin Odhiambo (Kenya): 8.4
- Soufiane Bayazid (Algeria): 7.6
Algeria imeonyesha ubora mkubwa katika hatua ya makundi, ikiingiza wachezaji watatu kati ya wanne wa kiufundi katika kikosi bora. Tanzania, Kenya, Burkina Faso, Guinea, na Sudan pia wameonesha vipaji vikubwa vinavyohitaji kufuatiliwa katika hatua za baadaye.
Kikosi hiki bora kinatoa mwangaza wa wachezaji wa kuvutia ambao wanaweza kuongoza timu zao kwenye hatua zinazofuata za CHAN 2025. Wapenzi wa soka wa Afrika wanatarajia ushindani mkali huku wachezaji hawa wakijaribu kuiongeza historia katika michuano hii.
Soma pia: CHAN 2025: Orodha ya wachezaji wanaolipwa Hela nyingi