Kama wewe ni mpenzi wa michezo ya kubashiri mtandaoni, basi bila shaka umeisikia au kuitumia Betway, moja ya tovuti maarufu za kubetia Tanzania. Ili kuanza kubet, hatua ya kwanza ni kufanya amana (deposit) kwenye akaunti yako ya Betway.
Jinsi ya kuweka hela Betway kwa kutumia mitandao ya simu
Katika makala hii, tutakuonyesha jinsi ya kuweka hela Betway kupitia mitandao yote mikubwa: M-Pesa, Airtel Money, Mixx by Yas (TigoPesa), na Halopesa.
1. Jinsi ya Kuweka Hela Betway kwa M-Pesa
M-Pesa ni mojawapo ya njia rahisi zaidi kwa watumiaji wengi Tanzania. Fuata hatua hizi:
- Nenda kwenye menyu ya M-Pesa kwa simu yako.
- Chagua Lipa kwa M-Pesa kisha Weka namba ya kampuni:
- Namba ya kampuni: 971772
- Ingiza Namba ya kumbukumbu: Tumia namba ya akaunti iliyosajiliwa Betway.
- Weka kiasi unachotaka kuweka.
- Weka PIN yako ya M-Pesa kuthibitisha muamala.
- Utaona ujumbe wa kuthibitisha na salio kuingia kwenye akaunti yako ya Betway mara moja.
2. Jinsi ya Kuweka Hela Betway kwa Airtel Money
Airtel pia ni chaguo jingine maarufu la kuweka hela Betway:
- Piga *150*60# kisha chagua Lipa Bili.
- Chagua Weka namba ya kampuni:
- Namba ya kampuni: 971772
- Ingiza namba ya kumbukumbu.
- Weka kiasi cha kuweka.
- Thibitisha kwa kutumia PIN yako ya Airtel Money.
- Muamala utakamilika papo hapo.
3. Jinsi ya Kuweka Hela Betway kwa Mixx by Yas (TigoPesa)
TigoPesa sasa inapatikana kupitia huduma mpya ya Mixx by Yas. Fuata hatua hizi:
- Fungua App ya Mixx au tumia menyu ya USSD *150*01#.
- Chagua Lipa Bili > Ingiza Namba ya Kampuni.
- Weka namba ya kampuni: 971772.
- Namba ya kumbukumbu.
- Weka kiasi na thibitisha kwa PIN yako ya Mixx/TigoPesa.
- Utapokea ujumbe wa kuthibitisha muamala wako.
4. Jinsi ya Kuweka Hela Betway kwa Halopesa
Halotel kupitia Halopesa pia inaruhusu malipo ya Betway kwa urahisi.
- Piga *150*88# kwenye simu yako.
- Chagua Malipo > Lipa Bili > Ingiza Namba ya Kampuni.
- Andika: 971772
- Namba ya kumbukumbu: Tumia namba ya simu ya Betway.
- Weka kiasi unachotaka kuweka.
- Thibitisha kwa kutumia PIN yako ya Halopesa.
Vidokezo Muhimu
- Hakikisha namba ya simu uliyosajili Betway ndiyo unayotumia kufanya malipo.
- Muamala unapaswa kuthibitishwa mara moja. Ikiwa utachelewa, wasiliana na huduma kwa wateja wa Betway.
- Hakikisha salio linatosha kabla ya kujaribu kufanya muamala.
Kuweka hela Betway sasa ni rahisi zaidi kwa kutumia mitandao yote maarufu nchini Tanzania kama M-Pesa, Airtel Money, Mixx by Yas (TigoPesa) na Halopesa. Fuata tu hatua tulizozieleza na uanze kufurahia kubashiri michezo, kasino na zaidi kupitia Betway.
Soma pia: