Katika dunia ya leo ya kidijitali, hakuna haja ya kusubiria foleni ili kulipia DSTV. Watumiaji wa Tanzania sasa wanaweza kulipia DSTV kwa simu online kwa urahisi kupitia mitandao mbalimbali ya simu kama M-Pesa, Airtel Money, Mixx by YAS (TigoPesa), na Halopesa.
Jinsi ya Kulipia DSTV mitandao yote ya simu
Huu ni mwongozo kamili wa jinsi ya kufanya malipo haya bila usumbufu:
1. Jinsi ya Kulipia DSTV kwa M-Pesa
Hatua:
- Piga *150*00#
- Chagua 4: Lipia bili
- Chagua 4: TV
- Chagua 1: DSTV
- Ingiza namba ya kumbukumbu (Smartcard number)
- Weka kiasi unachotaka kulipa
- Thibitisha malipo
Maelezo ya ziada: M-Pesa ni mojawapo ya njia rahisi na ya haraka zaidi ya kulipia DSTV, hasa kwa watumiaji wa Vodacom.
2. Jinsi ya Kulipia DSTV kwa Airtel Money
Hatua:
- Piga *150*60#
- Chagua 4: Lipa Bili
- Chagua 3: Malipo ya DSTV
- Weka namba ya Smartcard
- Weka kiasi
- Thibitisha malipo
Faida: Airtel Money inaruhusu malipo ya haraka na salama kwa DSTV moja kwa moja kutoka kwa simu yako.
3. Jinsi ya Kulipia DSTV kwa Mixx by YAS (TigoPesa)
Hatua:
- Piga *150*01#
- Chagua 4: Lipa Bili
- Chagua 3: TV
- Chagua DSTV
- Weka namba ya akaunti (Smartcard)
- Weka kiasi
- Thibitisha malipo
Mixx by YAS ni huduma mpya ya kisasa kutoka Tigo inayowezesha miamala ya aina mbalimbali, ikiwemo kulipia DSTV kwa simu online kwa urahisi.
4. Jinsi ya Kulipia DSTV kwa Halopesa
Hatua:
- Piga 15088#
- Chagua 4: Lipa Bili
- Chagua 3: DSTV
- Ingiza namba ya Smartcard
- Weka kiasi cha kulipia
- Thibitisha malipo
Maelezo: Halopesa inatoa suluhisho mbadala kwa watumiaji wa Halotel kulipia DSTV bila kutoka nyumbani.
Faida za Kulipia DSTV kwa Simu Online
- Urahisi: Huna haja ya kutoka nyumbani.
- Haraka: Malipo yanafanyika papo hapo.
- Usalama: Malipo yanathibitishwa mara moja kupitia ujumbe wa SMS.
- Upatikanaji: Unapatikana 24/7 kupitia mitandao ya simu.
Kulipia DSTV kwa simu online sasa ni rahisi zaidi kuliko hapo awali. Iwe unatumia M-Pesa, Airtel Money, Mixx by YAS (TigoPesa) na Halopesa.
Soma pia: