Unatumia Vodacom na hutaki kushangaa vifurushi vimeisha ghafla? Makala hii itakuonyesha jinsi ya kuangalia salio la vifurushi Vodacom kwa haraka, hata bila intaneti. Hakikisha unafuatilia hatua hizi ili kujua kilichobaki kwenye kifurushi chako cha internet, dakika, SMS, au kifurushi cha pamoja.
Hatua za Kuangalia Salio la Vifurushi Vodacom
Fuata hatua hizi rahisi bila kutumia intaneti:
- Fungua sehemu ya Kupiga Simu
- Ingiza *102#
- Bonyeza kitufe cha kupiga simu.
Angalia Taarifa Zako za Vifurushi
Utaona ujumbe wa menyu ukijitokeza ukionyesha:
- Salio la kifurushi cha intaneti
- Salio la dakika
- Salio la SMS
- Muda wa kuisha kwa kifurushi
Tumia App ya My Vodacom
Ikiwa unatumia simu janja (smartphone), unaweza kutumia App ya My Vodacom.
Hatua:
- Pakua My Vodacom App kutoka Play Store au App Store
- Jisajili kwa kutumia namba yako
- Fungua App na utaona salio la kifurushi lako moja kwa moja kwenye ukurasa wa mwanzo
Faida ya App: Unaweza pia kununua vifurushi, kuangalia historia ya matumizi na kupata ofa maalum.
Kuangalia salio la vifurushi Vodacom ni rahisi sana – chukua sekunde chache na piga *102#
kujua salio lako la dakika, SMS, au internet. Kwa watumiaji wa smartphone, app ya My Vodacom ni suluhisho la haraka na lenye taarifa zaidi.
Soma pia: