Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linapenda kuwataarifu vijana wote waliomaliza elimu ya sekondari na stashahada au shahada kutoka vyuo mbalimbali, kuwa fursa ya kujiunga na jeshi hilo imefunguliwa. JWTZ linawakaribisha vijana wenye uzalendo, maadili mema, afya njema na waliotayari kulitumikia taifa kwa uaminifu na uadilifu. Vijana watakaochaguliwa watapitia mafunzo maalum ya kijeshi kwa ajili ya kuwaandaa kulinda mipaka ya nchi, kushiriki katika operesheni za kulinda amani na kuchangia maendeleo ya taifa. Maombi yote yawasilishwe kwa kufuata taratibu zilizowekwa na kwa muda uliopangwa. JWTZ ni mwajiri anayetoa fursa sawa kwa wote bila kujali jinsia, kabila au dini.
Subscribe to Updates
Get the latest creative news from FooBar about art, design and business.
Previous ArticleMajina ya walioitwa kazini TFS na TAWA, 2025
Next Article Hukumu ya Kesi ya Utapeli